Utangulizi.
Mara nyingi mwanamke anapokosa hedhi japo kwa mwezi mmoja jambo ambalo humjia kichwani mwake ni kwamba huenda labda atakuwa mjamzito,anaweza akahisi kichefuchefu,kutapika ,maumivu kwenye maziwa/ anaweza akapata dalili zote za awali za uwepo wa ujauzito.
Baada ya kuhisi na kupata viashiria vya awali vya uwepo wa ujauzito ndipo huamua kununua kipimo na kujipima kabla ya kwenda kwa mtaalamu kutokana na vipimo kupatikana kwa urahisi kwa gharama nafuu,hata ivyo baada ya kupima majibu huonekana kuwa hana ujauzito.
Hapo ndipo swali lingine huibuka je ,majibu aliyo yapata ni sahihi au siyo sahii? Wazo linalo kuja baada ya hapo ni kwenda Katika kituo Cha kutolea huduma ili kupata kuhakikisha/kuthibitisha Kama majibu hayo ni sahihi au siyo sahii.
Ni kweli kabisa kuna wakati kipimo kinaweza kikaonesha hauna ujauzito wakati kiuhalisia una ujauzito na wakati mwingine kukosa hedhi lakini ukawa hauna ujauzito.
Kwa pamoja naomba fuatilia somo hili ili kupata kujua ni kitu gani ambacho huchangia kutokea kwa mambo haya yenye kuleta utatanishi.
Je Sababu gani hupelekea kipimo kioneshe hauna ujauzito licha ya kutokuona hedhi?
Kuna mambo kadhaa ambayo huweza kusababisha kipimo kitoe majibu hasi licha ya kuwepo kwa viashiria vyote vya ujauzito ,mambo hayo ni Kama ifuatavyo hapo chini:
.Kufanya kipimo mapema.
Mwili hauwezi kutengeneza kichocheo Cha mimba(human chorionic gonadotrophin) Kama bado mimba haijajishikiza kwenye ukuta wa mji wa mimba( uterus),mimba ikisha jishikiza kwenye ukuta wa mji wa mimba kondo la nyuma/ plasenta itaanza kuzalisha kichocheo Cha HCG.
Kwa kawaida toka mimba kutungwa huchukua takribani siku kumi hadi kumi na nne hadi kichocheo Cha mimba kuonekana kwenye mkojo.Kwaiyo endapo kipimo kitafanyika chini ya wiki mbili tangu kutungwa kwa mimba basi tegemea kabisa kupata majibu hasi hata kama unaujauzito,hushauriwa kupima mimba baada ya kukosa hedhi ya mwezi unao fuata.
.Kiwango kidogo Cha kichocheo Cha mimba kwenye mkojo(HCG).
Hushauriwa kupima mimba kwa Kutumia mkojo wa asubuhi kwa sababu kichocheo Cha mimba huwa kwa kiwango kikubwa kwenye mkojo wa asubuhi kuliko mkojo wa wakati mwingine.Mkojo wa asubuhi hukadiriwa kuchukua muda mrefu toka kukojoa kwa mara ya mwisho,kwahiyo endapo hautapima kwa Kutumia mkojo wa asuuhi Kuna uwezekano ukapata matokeo hasi licha ya kuwa na ujauzito. Kwahiyo Kama utaamua kupima mimba kwa kutumia mkojo ambao siyo wa asubuhi hushauriwa angalau kukaa masaa kadhaa bila ya kukojoa kisha ufanye kipimo.
.Mimba kutunga nje ya mji wa mimba.
Ni mara chache mimba hutungwa nje ya tumbo la uzazi mara nyingi kwenye mirija ya falopia inayo safirisha yai hadi kwenye mji wa mimba.Hali hii husababisha kuchelewa kuzalishwa kwa kichocheo Cha mimba,hivyo kuna uwezekano ukipima mimba kipimo kikaonesha hauna wakati unayo.Nenda hospitali ukafanyiwe uchunguzi endapo kipimo kinaonesha hauna ujauzito lakini una dalili hizi, Maumivu makali chini ya kitofu au upande mmoja,kutokwa na damu,kuhisi kichefuchefu na kutapika pia kupata Kizunguzungu.
.Kutumia kipimo ambacho kimeisha muda wake.
Kila kipimo kina muda maalumu ulio pangwa kitumike ,endapo kinatumika baada ya muda wake kuisha basi Kuna uwezekano mkubwa kikatoa majibu hasi ya uongo,vile vile kila kipimo huelezwa kiifadhiwe Katika mazingira flani mfano kuna baadhi ya vipimo huelezwa visi hifadhiwe Katika mazingira ambayo yana joto ridi kiwango fulani na endapo kikahifadhiwa Katika mazingira yasiyo takiwa ufanisi wa kutoa majibu sahihi hupungua,kwahiyo kabla huja nunua kipimo/ kabla huja kitumia kumbuka kuangalia muda kipimo kimetengenezwa na muda wa kuisha kufanya kazi.
.Makosa Katika Utumiaji.
Vipimo huwa na maelezo tofauti tofauti Jinsi ya kutumia kutokana na kampuni inayo tengeneza vipimo hivyo,kuna vipimo vingine ili vitoe majibu sahihi huitaji kiwango kidogo Cha mkojo kwahiyo endapo utatumia mkojo mwingi basi tegemea kupata majibu ya uongo,vile vile Kuna vipimo ambavyo vinahitaji mkojo mwingi ili vitoe majibu sahihi kwahiyo endapo utaweka mkojo kidogo Kuna uwezekano mkubwa wa kupata majibu yasiyo sahihi,kwahiyo ni vema kusoma au kuomba ushauri Jinsi ya kutumia kipimo husika kabla hujakitumia.
.Mimba ya mtoto zaidi ya mmoja.
Kichocheo Cha mimba huzalishwa kwa kiwango kikubwa kwa Mwanamke ambaye ana mtoto zaidi ya mmoja tumboni,kwaiyo kutokana na kichocheo Cha mimba kuzalishwa kwa kiwango kikubwa kwenye mkojo Kuna uwezekano kipimo kikashindwa kutoa majibu yasiyo sahihi.
.Mzunguko wa hedhi unao badilika badilika.
Kwa wale ambao mzunguko wao una badilika badilika Mara kwa mara ni ngumu Sana kutambua siku gani yai linaweza kupevuka na Kuna uwezekano wa kupata mimba,mara nyingi wenye mizunguko ya namna hii wanaweza kupata mimba bila ya kujijua,kwaiyo kutokana na kuto kujua wanaweza jikuta wanafanya kipimo kabla ya wakati na kuonekana hawana kumbe wana mimba.
Hata hivyo endapo ukafanya kipimo na ikaonekana hauna ujauzito na ukachelewa/ hauja pata hedhi uwezekano wa kuwa mjamzito haupo,hedhi inaweza kuchelewa kutokana na msongo wa mawazo au Magonjwa.
Kama kipimo kimeonesha hauna ujauzito na haujafanya kwa kuwahi yawezekana Kuna mambo kadhaa Katika mwili wako yatakuwa yamechangia usipate hedhi/ uchelewe kuona hedhi mambo hayo ni pamoja na:
. Unyonyeshaji.
Wakati wa kunyonyesha mwili hutengeneza kichocheo Cha prolactin ambacho husaidia kuzalisha Maziwa kwa wingi,kuzalishwa kwa kichocheo hiki kwa wingi husababisha mayai yasipevuke hivyo mwanamke anaweza asipate hedhi Kama ana nyonyesha kikamilifu au akachelewa kupata hedhi .
.Msongo wa mawazo.
Msongo wa mawazo unaweza sababisha kuvurugika kwa mfumo wa vichocheo vya mwili hivyo kusababisha mwanamke kukosa hedhi/kuchelewa kupata hedhi.
.Matumizi ya baadhi ya dawa.
Kila dawa huleta maudhi madogo kwa mtumiaji,kuna baadhi ya dawa zikitumika husababisha kukosekana kwa hedhi / kuchelewa kwa hedhi baadhi ya dawa hizo ni dawa za matibabu ya magonjwa ya akili.
.Mazoezi kupitiliza, husababisha kuvurugika kwa hedhi kutokana na matumizi makubwa ya nishati mwilini.
.Matumizi ya njia za uzazi wa mpango.
Ni kawaida Sana kwa Wanawake wanao tumia njia za kisasa za uzazi wa mpango kukosa hedhi au kuchelewa kupata hedhi.
Sababu zingine ni ,kuwa na uzito mdogo, kuwa na uvimbe kwenye tezi ya pituitary, uvimbe kwenye vifuko vya mayai,kubadilisha mazingira pamoja na aina ya chakula ambacho kinatumiwa.
Nini ufanye ili usipate majibu hasi ya uongo?
.Hakikisha unapima angalau baada ya kukosa hedhi ya mzunguko unao fuata.
.Hakikisha una tumia kipimo kwa usahihi kwa kufuata maelezo yaliyo tolewa na watengenezaji.
.Angalia kipimo Kama muda wake wa matumizi umeisha / bado kama umeisha usitumie badala yake kanunue kipimo kingine.
.Hakikisha unatumia mkojo wa asubuhi kujipima/ Kama hauto tumia basi angalau kaa kwa masaa kadhaa bila kukojoa kisha upime.
.Hakikisha haunywi maji mda mda mchache kabla ya kufanya kipimo ,kwasababu ukinywa maji utapunguza kiwango Cha kichocheo Cha mimba kilichopo kwenye mkojo.
Asante.
No comments:
Post a Comment