Utangulizi.
Matokeo chanya ya uongo yamekua yakileta athari kwa Wanawake wengi hususani kwa wale ambao wamekuwa wakihangaika kwa muda mrefu kupata ujauzito,Wanawake wengi hufurahi baada ya kupata matokeo chanya lakini furaha hiyo hupotea baada ya kutambua majibu aliyo yapata haya kuwa ya kweli.
Kwa upande mwingine matokeo chanya ya uongo yaweza leta athari kwa Wanawake ambao hawapo tayari kubeba ujauzito, habari njema ni kwamba ni mara chache Sana hutokea matokeo chanya ya uongo lakini hutokea.
Kwahiyo ni muhimu Sana kujua Jinsi kipimo kinavyo tumika ili kuweza kubaini matokeo tofauti ambayo yanaweza onekana Katika kipimo.
Kama nilivyo eleza awali,kipimo Cha mimba kwa kutumia mkojo ndicho kipimo ambacho hutumika zaidi kutambua ujauzito,pia kipimo hiki kinaweza kutumika na muhusika kutoka katika duka la dawa na kujipima Kama anahisi ana dalili ya ujauzito,vile vile kipimo hiki hutumika Katika kituo Cha kutolea huduma na mtaalamu wa maabara kutambua uwepo wa mimba.
Kipimo hiki hutambua kichocheo Cha mimba kwenye mkojo,kichocheo hiki huzalishwa na kondo la nyuma baada ya yai lililo rutubishwa kujishikiza kwenye ukuta wa mji wa mimba,Kama kichocheo Cha mimba kipo tayari kwenye mkojo kipimo kinaonesha mistari miwili ikimaanisha uwepo wa ujauzito ,pia Kama kichocheo hakipo kwenye mkojo kipimo kitaonesha mstari mmoja ikimaanisha si mjamzito.
Je ,nini huweza sababisha majibu chanya ya uwongo?
Kuna mambo kadhaa ambayo huweza sababisha kipimo kioneshe majibu chanya ya uongo,miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na:
.Mimba kuharibika.
Kwa kawaida kipimo Cha mimba kitaendelea kuonesha kuwa kuna ujauzito kwa muda fulani baada ya mimba kuharibika au kutoka.Wakati wa ujauzito utengenezaji wa kichocheo Cha mimba huongezeka kadiri mimba inavyo dhidi kukua,baada ya mimba kutoka/ kuharibika kichocheo Cha mimba hupungua taratibu Sana.Pia Kama mimba ilitoka yenyewe Kuna uwezekano baadhi ya mabaki kuendelea kutengeneza kichocheo Cha mimba kwahiyo ni bora kwenda hospitali kuchunguza Kama Kuna mabaki yoyote, kwahiyo Kuna uwezekano mkubwa Sana kupata majibu chanya ya uongo baada ya mimba kuharibika/ kutoka yenyewe.
.Matumizi ya dawa .
Matumizi ya dawa za matibabu ya uzazi yaweza sababisha kipimo Cha mimba kuonesha majibu chanya ya uongo,dawa za matibabu ya uzazi zina kichocheo Cha human chorionic gonadotrophin ndani yake ,kwahiyo Kutumia dawa hizo husababisha kichocheo hicho kuwepo kwenye damu pamoja na mkojo,kwahiyo Kama ulikuwa unatumia dawa hizi na ukahisi una mimba ni vema angalau kusubiri kwa muda wa wiki mbili Kisha ukapima.Dawa zingine ambazo zinaweza kuchangia kipimo Cha mimba kuonesha majibu chanya ya uongo ni dawa za Magonjwa ya akili mfano Xanax,varium,cpz , phenobarbital n.k,dawa zingine ni methadone,lasix , promethazine.
.Kukiacha kipimo kwa muda mrefu bila kusoma majibu.
Maelezo yaliyopo Katika pakiti ya kipimo yana maana kubwa sana Katika kutoa majibu sahihi,lakini endapo kipimo kitafanyika kinyume na maelezo Kuna uwezekano wa kupata majibu ya uongo. Kila kipimo Cha mimba kina maelezo ya muda ambao unatakiwa kusoma majibu kwahiyo endapo hujasoma majibu kwa muda ulio pangwa mkojo uliofyonzwa na kipimo hutoweka na matokeo yake baada ya kuonekana mstari mmoja itaonekana mistari miwili ,mstari wa pili unaweza ukawa hauonekani Sana au unaonekana kwa kufifia.Kwahiyo ili upate majibu sahihi ni lazima kuzingatia muda ulio pangwa mfano Kama unatakiwa kusoma majibu baada ya dakika mbili fanya ivyo,pia Kama ni dakika tano fanya ivyo.
.Kutumia kipimo kilicho isha muda wa matumizi.
Kipimo ambacho muda wake wa matumizi kikiendelea kutumika kinaweza sababisha kemikali iliyopo kwenye kipimo kutoa majibu ya uongo hasi,chanya au batili, Kwahiyo Kama unachukua jukumu la kujipima nyumbani hakikisha unaangalia muda wa matumizi wa kipimo Kama umepita au bado Kama umepita ni vema kununua kipimo ambacho muda wake haujaisha.
.Mimba kutungwa nje ya uzazi.
Wakati mwingine yai lililo rutubishwa laweza tungwa nje ya mji wa mimba,kuna mambo mbali mbali ambayo huchangia mimba kutungwa nje ya tumbo la uzazi ,baadhi ya Mambo hayo ni uwepo wa makovu kwenye mirija ya inayo safirisha yai kutoka kwenye mfuko wa mayai kwenda kwenye mji wa mimba, Maambukizi kwenye via vya uzazi,kufunga kizazi n.k,mimba iliyo tungwa nje ya tumbo la uzazi haiwezi tena kuwa mimba ya kawaida kwa kuwa hakuna sehemu ya mimba iyo kuendelea kukua hivyo basi itatakiwa kuondolewa kabla ya kuleta athari kubwa,japo kuwa mimba imejishika sehemu ambayo siyo ya kwake itazalisha kichocheo Cha mimba na ukipma mkojo itaonesha majibu chanya.
.Magonjwa.
Kuna baadhi ya Magonjwa yanaweza sababisha kupata majibu chanya ya uwongo ,Magonjwa hayo ni Kama Maambukizi ya bakteria Katika njia ya mkojo,Magonjwa ya figo ambayo husababisha kuwepo kwa seli za damu kwenye mkojo,uvimbe kwenye mfuko wa mayai hususani kwenye corpus luteum, matatizo Katika tezi ya pituitary japo yaweza tokea mara chache Sana.
.Mimba ya kikemikali.
Hii ni hali ambayo mimba iliyotungwa hukadiriwa kutoka yenyewe kabla ya wiki ya tano ya ujauzito.Wanawake wengi ambao hupata aina hii ya mimba huwa hawatambui kuwa ni wajawazito bali huchelewa kupata hedhi.
Mimba ya kikemikali huelezwa hutokana na yai lilito rutubishwa kuwa na matatizo ya chromosome,kwahiyo mwili wenyewe huitoa mimba pindi unapo tambua kuwa siyo sahihi.Japo yai lina kuwa hali jajishikiza moja kwa moja hutengeneza kichocheo Cha mimba hivyo basi ukipima mimba utapata majibu chanya ya uongo.
.Kutumia kifaa kichafu kuweka mkojo.
Mkojo ambao umewekwa kwenye kifaa ambacho siyo kisafi unaweza ukawa umechanganyika na vitu mbali mbali matokeo yake kipimo kitatoa majibu yauongo chanya/ hasi.
Nini ufanye ili usipate majibu chanya ya uongo unapo fanya kipimo nyumbani?
.Hakikisha unaweka mkojo kwenye chombo kisafi ambacho hakina kitu chochote ndani yake.
.Hakikisha hutumii kipimo ambacho wakati wake umepita badala yake tumika kipimo kingine.
.Soma majibu ndani ya muda ulio pangwa kutokana na kampuni iliyo tengeneza kipimo ,ikiweze ana kama ni dakika tano au mbili weka alamu ili muda ukifika usome majibu.
.Pia usipime mimba muda mfupi baada ya mimba kuharibika au kutoka yenyewe.
.Kama unatumia dawa za matibabu ya uzazi ni vema kupima mimba angalau baada ya wiki mbili tangu Kuacha Kutumia dawa izo.
.Mwisho kwa wale ambao wanashindwa/ wata pima na kupata majibu ni vema kwenda hospitali ili kuthibitisha kutoka kwa wataalamu wetu.
KARIBU.
No comments:
Post a Comment