Blog hii inahusika na utoaji wa elimu ya Afya ya Mama na mtoto na kutoa ushauri bure. Mawasiliano: 0712106789, 0753891441

Je ,umepanga kushika mimba?je wajua mambo gani ni muhimu kufanya kabla ya kushika mimba?

Utangulizi.

Yawezekana wakati huu wewe na mwenza wako mnapanga kupata familia/ mpo Katika mahangaiko ya kutafuta familia /pengine mnatarajia kupata familia hivi karibuni,lakini Kuna mambo kadhaa ambayo ni lazima uyafikirie kabla ya kufanya maamuzi ,Jambo la Kwanza ni lazima ufikirie mwenza wako atakuwa tayari kukubaliana na wazo lako,Jambo la pili mtindo wa maisha hauta athiriwa na mimba ambayo utakuwa nayo,tatu hali ya uchumi inaruhusu kuwa na familia  na ukailea Katika misingi iliyo bora, na wakati mwingine ni lazima ufikirie afya yako kama haitoweza kuleta athari kwako au mtoto wakati wa mimba,kujifungua/baada ya kujifungua.

Wakati wa ujauzito ni lazima ubadilishe mtindo wa maisha ambao ulizoeleka kuuishi kabla ya kupanga kuwa mjamzito/ wakati wa ujauzito kwasababu mambo mengi ambayo utayafanya Katika mwili wako huenda kuleta athari moja kwa moja katika mwili wako na mtoto pia.

Kwa maana hiyo tunajifunza ,kumbe mwanzo mzuri wa maisha bora ya mama na mtoto wake wakati wote wa ujauzito ,kujifungua na baada ya kujifungua una tegemeana na maamuzi ambayo wenza/ mwenza aliyafanya kabla ya kuamua kushika mimba,hivyo basi kama ulifanya maamuzi yasiyo sahihi basi  kuna uwezekano mama na mtoto wakapata matatizo wakati wa ujauzito,kujifungua au wasipate malezi bora,lakini kumbe ukifanya maamuzi sahihi leo kabla ya kupanga na mwenza wako kupata mtoto uwezekano wa mama na mtoto kupata matatizo katika kipindi chote cha cha ujauzito mpaka malezi huwa ni mdogo hivyo familia yako kuwa yenye afya bora.



Mambo ya kufanya kabla ya kushika mimba.

Najua wachache watakuwa wanatambua mambo haya hususani wale ambao washaingia kwenye familia lakini wengi wetu hatujui mambo haya ambayo ni msingi wakati wote wa ujauzito na malezi, mambo hayo ni:

.Acha Kutumia uzazi wa mpango.

Kama ulikuwa unatumia njia za kisasa za uzazi wa mpango ni wakati Sasa wa Kuacha Kutumia njia hizo,Kuna baadhi ya njia za kisasa za uzazi wa mpango huchukua muda mrefu kushika mimba baada ya Kuacha kuzitumia,hivyo kadiri utakavyo chelewa Kuacha Kutumia njia hizo ndivyo utakavyo chelewa kushika mimba.

.Onana na mtaalamu wa afya.

Kabla ya kubeba ujauzito ni vema zaidi kupanga na kuonana na mtoa huduma wa afya ili kushauriwa mambo mbali mbali, wakati mwingine ni muhimu kuonana na mtaalamu kabla kuliko kuonana na mtaalamu baada ya kushika mimba,hii huondoa athari ambazo zinaweza kuathirika afya ya mama na mtoto.

Kwa kawaida wajawazito wengi huudhuria kliniki kwa kuchelewa Sana hii husababisha kuchelewa kupata baadhi ya huduma za msingi kwa ukuaji wa mtoto, kwa kawaida kipindi Cha mwanzo Cha ujauzito ndicho kipindi ambacho uundaji wa viungo mbalimbali vya mtoto hufanyika hivyo mama akichelewa Kuna uwezekano mtoto kuzaliwa akiwa na mapungufu.

Kuonana na mtaalamu kabla ya ujauzito hulenga kutambua viashiria hatari kwa mjamzito na kuandaa jinsi ya kukabiliana navyo Katika wakati wote wa ujauzito mfano umri zaidi ya miaka 35,umri chini ya miaka 20 n.k,pia huduma hii hutoa hutoa fursa ya kupanga na kufanya maandalizi kabla ya ujauzito,vile vile hutoa fursa kwa wenza kupima afya zao kabla ya ujauzito ili kujua Jinsi ya kuwa saidia endapo watakuwa  na tatizo,Pia hutoa fursa ya mama kuanza matibabu ya dawa na virutubisho vya kumsaidia Mama kwa ujauzito ikiwa ni pamoja na kutibu Magonjwa ambayo yanaweza kuleta athari kwa mimba.

.Pata chanjo .

Kuna magonjwa mengi ambayo yanazuilika, ambayo Kama endapo hauta pata chanjo yanaweza kuathiri afya ya mama na mtoto,kwaiyo moja ya Mambo ambayo ni lazima kufanya  ni lazima kuhakikisha unapata chanjo.

.Panga bajeti yako.

Wakati wa ujauzito huwa haueleweki  kwa kuwa Kuna mambo mengi ambayo yanaweza jitokeza wakati wowote,hivyo basi ni vema kuanza kujiwekea akiba kidogo kidogo pindi tu mnapofikiria kushika mimba ili pesa hizo zipate kuwafaa wakati wowote itakapo tokea dharura.

.Badilisha mtindo wa maisha.

Kama ulikuwa unakunywa pombe,unavita sigara,hufanyi mazoezi ni wakati Sasa wa kubadili mtindo huo wa maisha na kuishi maisha ambayo hayato kuwa na athari Katika afya yako na mtoto atakaye kuwa tumboni.

Acha Kutumia pombe,unywaji wa pombe huathiri afya yako pamoja na mtoto tumboni,chemicali zilizopo kwenye pombe huingia moja kwa moja Katika mfumo wa damu na kuleta athari za moja kwa moja kwa mwanao,athari ambazo zinaweza jitokeza ni pamoja na mimba kuharibika, mtoto kufia tumboni,mtoto kuzaliwa akiwa na uzito mdogo,mtoto kuzaliwa akiwa mlemavu wa viungo vile vile mtoto anaweza kuzaliwa na ulemavu wa akili.

Acha Kutumia sigara,moshi ambao una tokana na sigara hutoa chemicali mbalimbali ikiwemo hewa chafu ya carbondioxide na nicotine,chemicali hizi pia huingia moja kwa moja katika mzunguko wa damu na kuathiri ukuaji na maendeleo ya mtoto,chemicali hizi zinaweza sababisha kupungua kwa usafirishaji wa hewa ya oxygen kwa mtoto hivyo mtoto kukosa hewa Safi,vile vile nicotine huongeza mapigo ya moyo na shinikizo la damu kwa Mama hivyo mama kuwa Katika hatari na kupata shinikizo la damu wakati wa ujauzito,pia chemicali hizi zaweza sababisha kupungua kwa usafirishaji wa virutubisho vya muhimu kwa mtoto hivyo afya ya mtoto kudorora. Sigara huongeza hatari ya mtoto kuzaliwa akiwa na matatizo Katika mfumo wa upumuaji mfano asthma,vile vile mtoto kuzaliwa mlemavu,kujifungua kabla ya wakati n.k,kwahiyo ni vema Kuacha Kutumia sigara kabla ya kujaribu kushika mimba na Kuacha Kutumia kabisa hata baada ya kujifungua kutokana na madhara niliyo yaeleza.

Anza kufanya mazoezi,kufanya mazoezi kabla ya ujauzito,wakati was ujauzito na baada ya kujifungua ni muhimu Sana,mazoezi kabla husaidia kuandaa mwili wako kupambana/ kukabiliana na mabadiliko yote ambayo hutokea wakati wa ujauzito,pia husaidia kuimarisha misuli ya mwili na kujenga stamina ili iwe rahisi wakati wa kujifungua pia mwili wako uweze kurudi kwa haraka zaidi Katika hali yake baada ya kujifungua,pia mazoezi humkinga mama dhidi ya kisukari ambacho hutokana na ujauzito.Kuna baadhi ya Wanawake hudhania wakati wa ujauzito ni wakati wa kupumzika tu hivyo hawatakiwi kabisa kujihusisha Katika mazoezi yoyote.Hata hivyo Kuna baadhi ya matatizo ambayo huitaji kufanya mazoezi kwa uangalizi au Kuacha kabisa kufanya mazoezi kutokana na athari ambazo zinaweza jitokeza, baadhi ya Mambo hayo ni pamoja na ugonjwa wa kisukari,ugonjwa wa kifafa,kuwa na historia ya kupata uchungu kabla ya wakati,mwenye historia ya kuharibika kwa mimba,shinikizo la damu,kondo la nyuma kujishikiza Katika njia ya kutokea mtoto n.k ,hivyo basi kabla ya kuanza kufanya mazoezi ni vema kuonana na mtaalamu ili aweze kukushauri mazoezi ambayo yatakufaa Kulingana na hali yako .

.Hakikisha una pata lishe bora.

Kula chakula bora haitakiwi tu wakati wa ujauzito pekee bali hata kabla na baada ya kujifungua,chakula bora wakati wa ujauzito husaidia kuupa mwili wako virutubisho bora kabisa tayari kwa kupokea ujauzito,siyo vema kushika ujauzito huku afya yako ikiwa imedhoofu kutokana na kukosa lishe bora kwasababu afya ya mtoto tumboni nayo itadhoofu kutokana na kukosa virutubisho vya msingi kutoka kwa mama.Vile vile kipindi Cha mwanzo ni kipindi muhimu Sana wakati wa ujauzito pia ni kipindi ambacho viungo vya  mtoto hutengenezwa hivyo kuhitaji zaidi virutubisho vya muhimu.

Pia wakati wa ujauzito  uhitaji wa chakula huongezeka kutokana na uwepo wa mtoto tumboni,kwahiyo utalazimika kuongeza idadi ya Milo ya chakula ambavyo vina kiwango Cha kutosha Cha madini ya chuma ,calicium na vitamini virutubisho hivyo ni muhimu Katika ukuaji na maendeleo ya mtoto.
Vile vile lishe bora husaidia uzalishaji wa maziwa ya kutosha baada ya kujifungua na kipindi chote Cha unyonyeshaji.Ulaji wa mboga mboga na matunda hushauriwa zaidi wakati wa ujauzito kwasababu ni vyanzo vikuu vya madini ya chuma na vitamini.

.Anza Kutumia folic acid.

Folic acid ni vitamin B9 ambayo hupatikana Katika baadhi ya vyakula pia hupatikana katika mfumo wa kidonge.Matumizi ya folic acid kabla ya ujauzito husaidia mtoto kuwa na afya bora,pia humsaidia mtoto asipatwe na upungufu wa damu.Kwaiyo Kama unatarajia kushika mimba ni muhimu Sana Kutumia vidonge vya folic acid angalau miezi miwili hadi miezi mitatu kabla ya kushika mimba hii husaidia mwili kuwa na kiwango Cha kutosha Cha vitamin B9 hivyo husaidia mtoto asizaliwe na tatizo la mgongo wazi(spinal bifida).Vile vile unaweza Kutumia vyakula ambavyo vina vitamini B9 lakini vyakula hivyo pekee havijitoshelezi kukupa kiwango Cha kutosha Cha vitamin hivyo ni lazima utumie vidonge mfano wa vyakula hivyo ni matunda(parachichi,machungwa ,papai n.k),mboga za majani,maharage,karoti n.k.
Licha ya kutumia folic acid kabla ya ujauzito ni lazima kuhakikisha unaendeleaje Kutumia dawa hizo Katika kipindi chote Cha ujauzito.


Kwa mambo mbali mbali yanayo husu  ujauzito,afya ya mama na mtoto karibu tukushauri.



Asante.
Share:

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Recent Posts