Watu wengi hudhania swala la kujua maendeleo ya ukuaji wa mtoto tumboni ni suala la mjamzito pekee Jambo ambalo siyo kweli bali hata mwanaume ni wajibu wake kutambua ukuaji wa mwanae ili aweze kutoa msaada wa haraka pale atakapo gundua kuna tatizo Katika ukuaji wa mwanae pia wakati ambao mama atakuwa pengine hawezi kufanya hata shughuli ndogo.
Kupitia makala hii utajifunza hatua ambazo mtoto hupitia hadi kuzaliwa kwake tangu mbegu ya kiume inapo kutana na yai na kutungisha mimba,nikusii fuatilia kwa makini makala hii ili angalau upate kujifungua machache Kati ya mengi ambayo nimekuandalia Katika makala hii.
Kutokea kwa ujauzito
Ili mimba iweze kutungwa ni lazima mbegu ya kiume kutoka kwa mwanaume mwenye afya njema na uwezo wa kutungisha mimba ikutane na yai kutoka kwa mwanamke mwenye afya bora na uwezo wa kushika ujauzito mara baada ya kujamiiana katika siku za hatari bila ya kutumia njia yoyote ya upangaji uzazi.
Wakati wa tendo la ndoa Mwanaume hukadiriwa kutoka mamilioni ya mbegu, lakini Kati ya mbegu hizo ni mbegu moja tu ambayo hutungisha mimba.Mwanaume hutoa mbegu za aina mbili,mbegu ya kiume na mbegu ya kike,kwa mantiki hii ni dhairi kabisa jinsia ya mtoto huweza kufaamika toka siku ya kwanza mimba inatungwa,kwahiyo kumbe mbegu za kiume ndizo ambazo huamua jinsia ya mtoto,baada ya mimba kutungwa yai lililo rutubishwa hujigawa kakita seli hai nyingi wakati linasafiri kuelekea kwenye tumbo la uzazi kujishikiza.
Maendeleo ya ujauzito Wiki ya nne .
Hiki ni kipindi ambacho endapo utaamua kujipima kwa Kutumia kipimo cha nyumbani ni dhahiri kabisa utapata majibu chanya.Pia ni wakati ambao sehemu mbali mbali za mwili wa mtoto huanza kutengenezwa sehemu hizo ni pamoja na moyo na mishipa ya damu,vile vile mtoto hutengeneza umbo la mwonekano wa sura pamoja na shingo.
Maendeleo ya ujauzito Katika wiki ya nane.
Wakati huu sehemu mbalimbali za mwili wa mtoto huendelea kutengenezwa,ngozi inayo funika macho huanza kutengenezwa, alama ya pua pia huanza kujitokeza kwa mbali,pia miguu na mikono vinakuwa vimetengenezwa lakini vidole ndo Kwanza vinaanza kujitokeza lakini vinakuwa bado vina utando Kama miuu ya bata ilivo.Pia wakati huu via vya uzazi vya nje hutengenezwa lakini bado jinsia ya mtoto inakuwa haijatambulika bado,moyo wa mtoto wakati huu unakuwa umeanza kudunda,kwa kawaida moyo huanza kudunda Katika wiki ya sita ya ujauzito.
Maendeleo ya ujauzito Katika wiki kumi na mbili.
Wakati huu mtoto anakuwa ameanza kucheza kwa mbali Sana japo siyo rahisi mama kutambua,pia mapigo ya mtoto yanaweza kusikika daktari au mkunga wako anaweza kusikiliza mapigo ya mwanao kwa Kutumia kifaa maalumu. Vile vile sehemu za Siri zinakuwa zishajijenga vyema Katika wakati huu hivyo basi unaweza kutofautisha kwa mwonekano wa nje,pia mtoto anakuwa ameanza kukojoa lakini Kuna uwezekano usionekane ndani ya mfuko wa uzazi(plasenta),pia ngozi ya macho hujifunga ili kuya Linda macho ambayo yanaendelea kutengenezwa.
Maendeleo ya ujauzito Katika wiki ya kumi na sita.
Wiki hii mtoto anakuwa anauwezo wa kuchezesha macho,moyo pamoja na mishipa ya damu vinakuwa vimekamilika, vidole pia vina kuwa vimeanza kutengeneza michirizi.Pia figo na kibofu Cha mkojo vinakuwa vinafanya kazi kikamilifu Kama ambavyo Inaweza ikathibitishwa na uwepo wa mkojo kwenye maji yanayo mzunguka mtoto.
Maendeleo ya ujauzito wiki ya ishirini.
Kipindi hiki mtoto anakuwa na uwezo wa kujinyoosha na kunyonya vidole,wakati huu pia mtoto anakuwa anacheza tumboni mwa mama ake pia mama anakuwa na uwezo wa kumsikia,vile vile wakati huu mtoto huonekana vizuri kwahiyo Kama ulikuwa unahitaji kufanya utrasound huu ni wakati mzuri,pia wakati huu unaweza kutambua jinsia ya mwanao kupitia kipimo Cha utrasound.wakati huu pia mkunga au daktari wako anaweza kusikiliza mapigo ya moyo ya mtoto wako kwa Kutumia kifaa Cha kawaida,utando unao fanana na maziwa hutanda Katika ngozi ya mtoto, vile vile nywele za mtoto huanza kutengenezwa .
Maendeleo ya ujauzito wiki ya ishirini na nne.
Kipindi hiki mfumo wa masikio wa mtoto unakuwa umeundwa kikamilifu na unafanya kazi hivyo basi mtoto huwa na uwezo wa kusikia sauti na kuweza kufuata uelekeo ambao sauti inatokea.Watoto huweza kutambua sauti wawapo tumboni na kujenga mazoea na sauti ambazo huzisikia Mara kwa Mara hivyo huwa rahisi kwao kuzitambua baada ya kuzaliwa.
Maendeleo ya ujauzito wiki ya ishirini na nane.
Kutokana na taratibu za uzazi zilizowekwa na wizara ya afya mtoto akizaliwa chini ya wiki ya ishirini na nane huchukuliwa mimba imeharibika na halkuna uwezekano wa mtoto kuishi,lakini endapo mtoto atazaliwa kuanzi wiki ya ishirini na nane Kuna uwezekano wa mtoto kuishi. Pia ni muda wa kujifunza nini unatakiwa kufanya pia nini hutakiwi kufanya ukiwa Katika chumba Cha uzazi,jinsi ya kumuhudumia/ kumlea mtoto wako ikiwa ni pamoja na kumnyonyesha mtoto na kutambua viashiria vya hatari kwa mtoto wako.Pia Kuanzia wakati huu unashauriwa kutembea na taarifa zako zote za uzazi popote unapo kwenda kwasababu unaweza kupatwa na uchungu wakati wowote ili uweze pata msaada kwa urahisi.Wakati huu mtoto huanza kufumbua macho.
Maendeleo ujauzito wiki thelathini na mbili.
Wakati huu mifupa ya mtoto inakuwa ishaundwa kwa ukamili lakini bado inakuwa laini,mtoto hufungua na kufumba macho Kulingana na mabadiliko ya mwanga,pia mwili wa mtoto huanza kuhifadhi madini muhimu Kama vile madini ya chuma pamoja na calcium,vile vile nywele laini zilizo jitokeza Katika mwili wa mtoto hutoweka,pia hadi kufikia wakati huu kichocheo Cha prolactin kinakuwa kishafanya maandalizi ya kutosha ya kutoa maziwa pindi mtoto atakapo zaliwa hivyo basi kuanzia wakati huu mama unaweza ukaanza kuona majimaji ya njano Katika chuchu zako hivyo usishangae uonapo hali hii.
Maendeleo ujauzito wiki ya thelathini na sita.
Wakati huu mtoto hugeuka kichwa chake huelekeza Katika mlango wa kizazi tayari kwa kujifungua.Wiki ya thelathini na Saba huchukuliwa Kama ni wakati mwafaka wa mtoto kuzaliwa japo Kuna wengine wanaweza wasijifungue wakati huu badala yake wakajifungua Katika wiki ya 38,39 hadi wiki ya 40
Kujifungua.
Safari ya ujauzito huishia Katika wiki ya arobaini japo kuna ambao wata jifungua kabla ya muda huu na wengine wanaweza wakapitiliza hadi wiki ya arobaini na mbili, tarehe ya kujifungua hukadiriwa kutoka katika siku yako ya Kwanza ya kupata hedhi kwa Mara ya mwisho hivyo basi kunawengine wanaweza bahatika kujifungua Katika tarehe iyo pia wengine wanaweza wasijifungue Katika tarehe hiyo,lakini kwa kawaida unaweza kujifungua wiki moja au mbili kabla ya tarehe ya matazamio au wiki moja au mbili baada ya tarehe ya matazamio .
No comments:
Post a Comment