Blog hii inahusika na utoaji wa elimu ya Afya ya Mama na mtoto na kutoa ushauri bure. Mawasiliano: 0712106789, 0753891441

Je wajua mimba hutungwaje?





UTUNGAJI MIMBA

Ili mimba iweze kutungwa ni lazima mbegu ya kiume kutoka kwa mwanaume mwenye afya njema na uwezo wa kutungisha mimba ikutane na yai kutoka kwa mwanamke mwenye afya bora na uwezo wa kushika ujauzito mara baada ya kujamiiana katika siku za hatari bila ya kutumia njia yoyote ya upangaji uzazi.

Pia kukamilika kwa zoezi hili hutegemeana na kutokea kwa hedhi au kwa namna nyingine ili mimba iweze kutungwa nilazima hedhi itokee kwanza.


Nini maana ya hedhi ?

Hedhi ni mpangilio wa mabadiliko yanayotokea kwa mwanamke ili kuuweka mwili tayar kwa kuupokea ujauzito.

Moja ya viungo vya uzazi vya mwanamke kijulikanacho kama ovari(kifuko cha mayai) kila mwezi huachilia yai moja ambalo hurutubishwa na mbegu ya kiume kama ngono isiyo salama itafanyika kitendo hiki kitaalamu hujulikana kama ovulation.Hali hii hutokea tu kwa wakina mama ambao wana mzunguko unaopevusha mayai( ovulatory circle).
Kuna baadhi ya akina mama hupata mabadiliko kama kawaida isipo kuwa kutokana na matatizo katika vifuko vya mayai ,yai huwa haliachiliwi  hali hii hujulikana kama unovulatory circle ,yaani mzunguko usiopevusha mayai kwaiyo ni ngumu sana mimba kutungwa kwa wakina mama ambao wana aina hii ya mzunguko.

Kwaiyo mara baada ya hedhi kutokea mabadiliko huanza tokea tena katika mfuko wa uzazi ikiwa ni pamoja na kutengenezwa kwa moja ya kuta katika tumbo la uzazi endometrium mabadiliko haya husaidiwa na vichocheo vya uzazi.

Soma,vidonda-vya-tumbo.html

Je,mimba hutungwa lini?

Katika siku za hatari za mzunguko wa mwanamke yai huachiliwa kutoka katika kifuko cha mayai,yai husafiri hadi kwenye mirija ya uzazi na endapo litakutana na mbegu ya kiume mimba hutungwa.
Kipindi cha kujamiana mwanaume hutoa mbegu nyingi sana lakini kati ya izo ni mbegu moja tu hutungisha mimba,kwa kawaida mimba kutungwa hufanyika kati ya masaa 24 hadi 48 baada ya yai kuachiliwa kutoka kwenye kifuko cha mayai kwaiyo wanandoa tunashauriwa kukitumia vizuri kipindi hiki kama tunataka kupata mtoto.Kwaiyo baada ya utungwaji wa mimba safari huendelea hadi kwenye mji wa mimba ambako mimba itaendelea kukua,safari hii huchukua takribani siku tatu hadi nne. Kujishikiza kwa mimba katika kuta za uzazi hukamilika baada ya siku 11 tangu upevushaji wa mayai ulipo fanyika.
Baada ya hapo mimba huendelea kukua hapo hadi muda wa kujifungua unapofika.




Karibu mikathommedia  uelimike nasi na kupewa ushauri wa bure juu ya afya yako.


Kwa maoni ,ushauri ,usikose kutuandikia kupitia mikathom41@gmail.com .

Karibu sana.



Share:

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Recent Posts