Kondomu.
Kondomu ni njia pekee ya uzazi wa mpango ambayo hufanya kazi mbili kwa Wakati mmoja,kondomu huzuia mwanamke kupata mimba vile vile huwa kinga watumiaji dhidi ya Magonjwa ya ngono.
Kondomu zimegawanyika Katika makundi mawili nayo ni:
.Kondomu ya kiume.
.Kondomu ya kike.
Jinsi inavyo fanya kazi.
Kondomu ya kiume/kike hufanya kazi kwa kuzuia mbegu za kiume kuingia Katika via vya uzazi wa mwanamke,vile vile uzio husababisha wadudu waliopo Katika sehemu za Siri za mwanamke kushindwa kumpata mwanaume na kinyume chake hivyo kuwa Kinga wasipate Magonjwa ya ngono na Maambukizi ya virusi vya UKIMWI.
Kondomu ya kiume.
Ni mpira laini ambao mwanaume huu visha Katika uume ulio simama Wakati wa tendo la ndoa.
Faida ya kutumia kondom
.Hupatikana kwa urahisi vile vile yeyote anaweza akatumia kwa kufuata maelezo bila kumhusisha mtoa huduma za afya.
.Kondom haina maudhi madogo ambayo utokana na uwepo wa vichocheo.
.Inaweza ikatumika Kama njia ya ziada ya uzazi wa mpango kwa muda mfupi.
.Uzazi hurudi kwa haraka Sana,mara tu mtumiaji atakapo acha Kutumia uwezekano wa kupata mimba huwa mkubwa.
.Ina wakinga watumiaji dhidi ya Magonjwa ya ngono na virusi vya UKIMWI.
.Haihitaji matumizi ya kila siku bali huwakinga watumiaji Wakati wanapo hitaji Kutumia.
.Huzuia mimba kwa kiwango kikubwa.
.Haihitaji elimu ya kutosha ili kuitumia.
.Ni salama.
Ufanisi
Ufanisi wa kondomu hutegemeana na uwezo wa mtumiaji Kutumia kwa usahihi na Mara kwa mara Katika kila tendo.
Kwaiyo uwezekano wa kupata Magonjwa ya zinaa na kuzuia mimba huwa ni mkubwa zaidi Kama ikitumika kwa usahihi.
Mara chache mimba au Magonjwa ya zinaa yanaweza patikana kutokana na kuvutika kwa kondom au kupasuka.
Endapo ikitumika kwa usahihi Katika kila tendo Kati ya Wanawake 100 Wanawake 98 hawato pata mimba Wanawake 2 pekee watapata mimba.
Isipo tumika kwa usahihi Katika kila tendo Kati ya Wanawake 100 Wanawake 85 hawato pata mimba ,Wanawake 15 pekee watapata mimba.
Nani anaweza tumia/ Nani asitumie?
Wanaume /wanawake wote wanaweza kutumia kondom isipo kuwa kwa wale ambao wana mzio na mpira ulio tumika kutengeneza kondom, hawa hushauriwa Kutumia njia nyingine ya upangaji wa uzazi endapo watakuwa hawana Maambukizi ya Vvu na Magonjwa ya ngono.
Vile vile Wanawake ambao wanatumia dawa ya miconazole au econazole ya kujiingizia ukeni ili kuondoa bakteria ukeni hawashauriwi Kutumia kondom kwakuwa dawa Inapunguza ufanisi wa kondomu badala yake hushauriwa Kutumia kondomu ya kike au kutumia njia nyingine ya uzazi. Lakini endapo wanatumia vidonge vya kumeza kutibu wadudu ukeni wanaweza wakatumia kondomu.
Kurudi kwa uzazi
Mara mtumiaji anapoacha kutuma kondomu uwezekano wa kutungisha mimba huwa mkubwa.
Jinsi ya Kutumia.
.Hakikisha unatumia kondomu mpya Katika kila tendo la ngono,lakini kabla ujatumia unashauriwa kuichunguza vizuri Kama muda wake wa matumizi umepita au bado Kama muda wa matumizi umepita usiitumie,vile vile usitumie Kama imechsnika au kuharibiwa.
.Fungua kondom kwa kuangalifu bila ya kutumia meno ,kucha au kitu chochote chenye kuharibu kondomu.
.Hakikisha unavisha kondomu kwenye uume ulio simama kabla ya kugusa sehemu za Siri za mwenza wako,hakikisha unakandamiza kwa kidole kwenye kichwa Cha kondom kabla ya kuvaa ili hewa isiingie.
.Ukisha weka kondomu katika kichwa Cha uume viringisha taratibu kuelekea kwenye shina la uume,Kama kondomu inakuwa ngumu Kuiviringisha yawezekana umegeuza Kama haipo nyingine geuza na uviringishe.
.Mara baada ya kufika mshindo toa uume katika uke huku ukiwa umesimama Kisha viringisha kondomu kutoka kwenye shina la uume bila kumwaga shahawa Kisha viringisha kondomu kwenye pakiti na tupa kwenye chombo Cha taka.
.Kama utarudia kufanya tendo hakikisha unatumia kondomu mpya tena,epuka Kutumia kondomu moja Mara mbili.
Mambo usiyotakiwa kufanya Wakati wa Kutumia kondomu.
Baadhi ya Mambo yakifanywa huweza sababisha kondomu kuchanika hivyo ni vema kuyaepuka mambo ayo:
.Epuka Kuiviringisha kondomu Kwanza kabla ya kuivisha kwenye uume.
.Usitumie mafuta kulainisha kondomu kwasababu mafuta huweza haribu mpira uliotumika kutengeneza kondomu.
.Usitumie kondomu ambayo rangi yake haieleweki au imebadilika.
.Usitumie kondomu ambayo kilainishi /mafuta yake yamekauka .
.Usitumie kondomu moja katika matendo mawili ya ngono ,kondomu mpya itumike katika kila tendo.
.Vile vile usitumie kondomu moja kufanya ngono katika njia tofauti tofauti mfano mdomoni,njia ya haja kubwa Kisha ukeni kwa kufanya I've utahamisha vimelea vya Magonjwa kutoka sehemu moja hadi nyingine.
Karibu tukushauri.
No comments:
Post a Comment