Pelvic inflamatory disease(pid).
Ni maambukizi katika via vya uzazi vya mwanamke shingo ya kizazi (cervix) maambukizi katika sehemu hii kitaalamu huitwa cervicititis ,nyama za mji wa mimba( endometrium) maambukizi haya kitaalamu huitwa endometritis,na mirija ya uzazi (fallopian tubes) maambukizi haya kitaalamu huitwa salpingitis.Maambukizi haya katika miaka ya karibuni yamekuwa yakiwasumbia wanawake wengi kote duniani na kujikuta wakihangaika huku na kule ili kupata suluhu la tatizo hili.
Je,nini chanzo cha tatizo hili la pid?
Kuna vimelea wengi ambao wanaweza wakasababisha ugonjwa huu lakini visababishi zaidi vya ugonjwa huu vinatajwa ni vimelea vinavyo sababisha ugonjwa wa kisonono(neiseria gonorrhoae) na vimelea aina ya chlamydia trichomatis.
Je ni vipi ugonjwa huu huenea?
Wanawake wengi hujikuta wanapatwa na vimelea vinavyo sababisha maambukizi katika via vya uzazi kutokana na njia tajwa hapo chini.
.Kuwekewa moja ya njia ya uzazi wa mpango(vipandikizi) kitaalamu IUCD ndani ya mji wa mimba ambako huweza sababisha vimelea kupenya kirahisi na kuvishambulia viungo ivo.
.Utoaji mimba usio salama( post abortal) au mara baada ya mimba kutoka (miscarrage).
.Ngono isiyo salama na mtu ambaye anavimelea vya gonorrhea au trichomatis.
.Maambukizi mara baada ya kujifungua (post partum period).
.Damu yenye vimelea vya pid.
Je wepi wapo katika hatari ya kupata ugonjwa wa pid?
.Watu wenye wapenzi zaidi ya mmoja.
.Kufanya ngono isiyo salama.
.Kuwahi kuugua ugonjwa huu kabla au kuwa na magonjwa ya zinaa.
Je utajuaje kama una ugonjwa wa pid?
Kuna viashiria vingi ambavyo vinaweza vikaonesha umepatwa na maambukizi katika via vyako vya uzazi ,viashiria ivyo ni pamoja na
.Maumivu makali wakati wa tendo la ndoa.
.Kuhisi homa.
.Kuhisi kichefuchefu na kutapika.
.Maumivu wakati wa kukojoa.
.Maumivu ya tumbo hasa chini ya kitovu.
.Maumivu ya mgongo.
.Kutokwa na uchafu kwenye tupu ya mwanamke,uchafu huu huambatana na harufu mbaya
.Kutokwa na damu wakati wa hedhi bila mpangilio maalumu.
Vipimo
Vipimo ambavyo vinaweza fanyika ili kugundua kama mama amepata vimelea vya ugonjwa huu ni pamoja na.
.Kupima mkojo kwa darubini ili kujua vimelea waliosababisha maambukizi
.Kuchukua utando unaozunguka shingo ya uzazi ili kubaini ni jamii gani ya vimelea vimesababisha maambukizi
.Kupima magonjwa ya ngono ikiwemo Hiv.
.Utrasound ya nyonga ili kubaini kama kuna maambukizi katika njia ya uzazi.
Matibabu
.Awali yoyote unashauriwa mara unapo jihisi una maambukizi ya ugonjwa huu usitumie dawa holela unashauriwa kumwona daktari au mtaalamu yeyote wa afya.
.Dawa aina ya ant biotics hutumika kuwaua wadudu waletao vimelea vya pid,dawa zinazoshauriwa kutumia kutokana na mwongozo wa wizara ya afya ni pamoja na ,doxline pamoja na cefotetan,clindamycin pamoja na gentamycin,ampicilin na sulbutan pamoja na doxiline,na cefriaxone ai cefotetan na doxiline
Madhara ya sababishwayo na pid
.Kutokea makovu katika njia ya uzazi.
.Mimba kutungwa nje ya tumbo la uzazi kitaalamu ectopic pregnancy ,hali hii hutokana na yai lililokwisha rutubishwa kushindwa kuendelea na safari ya kwenda kujishikiza kwenye kuta za tumbo la uzazi kutokana na makovu,matokeo yake mimba huendelea kulua hapo na mgonjwa huitaji matibabu ya dharura ili kunusuru uhai wake.
.Ugumba,Kutokana na vimelea kuharibu na kushambulia via vya uzazi na kusababisha kukosekana kwa mimba,pia kuchelewa kupata matibabu huongeza hatari ya mama kuwa mgumba.
.Maumivu sugu ya kiuno kutokana na uwepo wa makovu kweny mirija ya uzazi na viungo vingine.
.Kukusanyika kwa usaha kwenye njia ya uzazi na kifuko cha mayai
Je,nitajikingaje dhidi ya ugonjwa wa pid?
.Kuhakikisha unafanya ngono salama au unatumia kondom kwa usahihi katika kila tendo au kama utashindwa ni vema kuacha kabisa ngono
.Kuhakikisha unafanyiwa vipimo vya afya mara kwa mara katika mfumo wa uzazi na magonjwa ya zinaa.
.Kupata ushauri kutoka kwa wataalamu wa afya mara tu unapoanza kuona dalili tofauti na kupata matibabu.
.Kuhakikisha unakuwa na mpenzi mmoja au kuwa mwaminifu kwa mwenza wako.
.Kuhakikisha hufanyi mapenzi mara baada ya kujifungua,mimba kuharibika,kutoka ili kuhakikisha shingo ya uzazi inakuwa vema.
No comments:
Post a Comment