Blog hii inahusika na utoaji wa elimu ya Afya ya Mama na mtoto na kutoa ushauri bure. Mawasiliano: 0712106789, 0753891441

Mambo ambayo huatarisha figo yako!!!

Figo

Figo ni moja kati ya viungo muhimu katika mfumo wa utendaji kazi katika mwili wa binadamu, kwa kawaida kila binadamu anafigo mbili ,moja katika upande wa kulia na nyingine katika upande wa kushoto,umbile halisi la figo ni kama maharage na yamejificha nje ya utando unaozunguka tumbo chini kidogo ya mbavu za chini.




Je figo hufanya kazi gani?

.Kazi kubwa ya figo ni kuchuja vitu mbalimbali ikiwemo sumu ambazo hupatikana kwenye damu Mara baada ya kuvunjwa vunjwa na ini, kwahiyo figo husaidia kuhifadhi na kudhibiti kiwango cha maji na madini mwilini,ili kuhakikisha kazi iyo inafanyika vizuri figo huchuja vitu ambavyo vipo kwenye damu na maji ambayo yapo mwilini na kuzitoa sumu izo kwa njia ya mkojo, pia huchuja maji yasiyo hitajika na kunyonya madini na chemikali muhimu na kuzirudisha katika mzunguko wa damu.

.Pia figo husaidia katika utengenezaji wa erythropoietin ambacho ni muhimu katika utengenezaji wa seli nyekundu za damu.

.Figo husaidia katika uzalishaji au utengenezaji wa vitamini D ambayo ni muhimu mwilini.

.Husaidia katika kuthibiti na kurekebisha shinikizo la damu mwilini.

.Husaidia kurekebisha au kuthibiti kiasi cha vitu mbali mbali katika damu pamoja na kiwango cha maji yanayo hitajika katika mwili.




Soma pia:kuto-kupata-hedhi-husababishwa-na-nini.html



Mambo hatarishi kwa figo yako.

Pamoja na figo kufanya kazi kubwa ya kuhakikisha mwili haupati madhara kutokana na uwepo wa sumu kwenye damu ,kuna baadhi ya mambo ambayo sisi wanadamu huyafanya kwa ajili ya starehe,au uzembe  aiza kwa kujua madhara yake baadae au kwa kuto kujua madhara ambayo yanaweza yakajitokeza katika siku za baadae, mara nyingi athari hizo huanza kidogo kidogo lakini kadiri mtu anavyodhidi kurudia kitendo basi ndivyo athari katika mafigo inapoongezeka hadi kufikia kipindi figo kushindwa kufanya kazi kabisa na kusababisha kifo.

Mara nyingi figo inapopunguza utendaji kazi au kushindwa kufanya kazi vizuri husababisha  sumu ambazo ilibidi zitolewe nje kupitia mkojo aiza zitolewe kidogo au zisitolewe kabisa ,ivyo kusababisha kuwa na mkusanyiko au mlundikano wa sumu hizo mwilini sumu hizo ni pamoja na urea. Kuongezeka kwa kiwango cha sumu hizo husababisha kuiongezea kazi figo  na baadae kushindwa kufanya kazi na kupelekea kutokuwepo kwa uwiano wa maji mwilini .Kwaiyo athari kwenye figo husababishwa na:

.Uvutaji sigara.

Chemikali ambazo hupatikana kwenye sigara husababisha athari kwenye mishipa ya damu ikiwa na pamoja na mishipa iyo kuwa migumu ivyo kupungua ufanisi wa utendaji kazi wa mishipa iyo,ugumu wa mishipa husababisha kupungua kwa kiwango cha damu safi kwenye figo, ivyo kupelekea kupungua kwa utendaji kazi wa figo, kwaiyo kadiri mtumiaji wa sigara atakavyokuwa anaendelea kutumia itapelekea utendaji kazi wake kupungua taratibu na matokeo yake figo itashindwa Fanya kazi kabisa.


Kwaiyo kwa wale ambao ni watumiaji wa sigara wanashauriwa kuacha kutumia kabisa au kutumia mara chache zaidi kama itashindikana ili kuepuka madhara yatakayojitokeza baadae kwenye figo.


.Kutokunywa maji ya kutosha.

Maji hufanya kazi nyingi mwilini ikiwemo kusaidia kutoa sumu mwilini,kwahiyo kutokunywa maji kwa wingi husababisha kukusanyika na kugandamana kwa sumu hizo mwilini,kadiri sumu izo zinavyo zidi kubaki mwilini ndivyo zinavyo zidi kuleta madhara kwenye figo.


Kwaiyo tunashauriwa kunywa maji mengi mara kwa mara ili kuondoa mkusanyiko wa sumu mwilini na kuipunguzia kazi ya kutoa taka mwili figo.


.Kuto kukojoa mara kwa mara hata kama kibofu kimejaa.

Kuto kukojoa kwa wakati husababisha mkojo kurudi na kufyonzwa tena na figo matokeo yake figo inajaa maji,pia husababisha kuongezeka kwa msukumo wa mkojo ndani ya kibofu ambako baadae husababisha figo iyo kuongezeka ukubwa na kuanza kukandamiza viungo jirani hali hii husababisha figo kushindwa kufanya kazi.

Hivyo tunashauriwa kukojoa mara kwa mara pindi tu tunapo hisi kibofu kimejaa.

.Matumizi ya chumvi kwa kiwango kikubwa.

Chumvi ina madini ya sodium ambayo huitajika kiasi kwa matumizi mbali mbali mwilini, madini haya pindi yanapotumika husababisha kuongezeka kwa msukumo wa damu ambao huleta athari katika figo,pia husababisha maji kubakizwa mwilini kwa kiwango kikubwa.


Hivyo basi ili kuondoa athari ya figo itokanayo na matumizi ya chumvi kwa wingi tunashauriwa kutumia chumvi kwa kiasi katika chakula.

.Matumizi holela ya dawa hususani dawa za kutuliza maumivu.

Dawa za kutibu magonjwa licha ya kutibu ugonjwa husika huleta maudhi madogo madogo, kwaiyo dawa za kutuliza maumivu licha ya kufanya kazi iyo huleta athari kwenye figo .Dawa izo ni pamoja na ibrufen.Kwaiyo pindi unapo patwa na tatizo unashauriwa usipende kutumia dawa ovyo bila kupata ushauri kutoka kwa daktari ili kuepuka au kupunguza athari zinazo weza tokana na matumizi ya dawa izo.

.Kuwa mnene kupitiliza.

Unene kupitiliza unaweza ukatokana na kula mlo ambao siyo sahii na kiwango kisicho sahii ,pia waweza sababishwa na kuto kufanya mazoezi mara kwa mara,mara nyingi watu wanene katika mishipa yao ya damu huwa kuna mafuta mengi ambayo husababisha kupungua kwa kipenyo cha mishipa iyo,kupungua kwa kipenyo katika mishipa husababisha kuwepo kwa msukumo mkubwa wa damu ambao unaweza ukaathiri figo.

Kwaiyo ili kupunguza uzito basi tunashauriwa kufanya mazoezi ya viungo kwa kiasi na kuhakikisha mlo ambao unakula ni sahihi na kwa kiwango sahihi.

.Matumizi ya pombe kupitiliza.

Matumizi ya pombe mara kwa mara huleta athari nyingi katika mwili wa binadamu ikiwemo athari katika kiungo ambacho huzalisha insulini ambayo hudhibiti kiwango cha sukari mwilini ,kuathirika kwa kiungo hiki husababisha kiwango kikubwa cha sukari kuwepo kwenye damu ,kiwango kikubwa cha sukari huleta athari katika vifuko vya kuchuja mkojo ivyo kuathiri utendaji kazi wa figo na figo inaweza fika wakati ikashindwa Fanya kazi kabisa kutokana na matumizi ya mara kwa mara.

Kwaiyo tunashauriwa kuacha au kupunguza matumizi ya mara kwa mara ya pombe ili kuipunguzia kazi figo ambayo baadae inaweza ikapata athari.

.Matumizi ya sukari kupitiliza.

Matumizi makubwa ya sukari huongeza uwezekana mkubwa wa kupata kisukari,sukari inapokuwa nyingi kwenye damu vifuko vya kuchuja uchafu kwenye figo hupata athari na kusababisha kuwepo kwa protein kwenye mkojo huo.Kuna baadhi ya watu ambao hupata tatizo la figo kutokana na kisukari figo zao hushindwa kufanya kazi kabisa.

Kwaiyo tunashauriwa kubadili mtindo wa maisha ambao unaweza ukasababisha tukapata kisukari ambacho huleta madhara makubwa katika figo.


.Kukosa usingizi.

Baadhi ya tafiti zimeonesha kwamba kipindi mtu anavyo kuwa amelala ndio muda ambao majeraha ambayo yalitokea kwenye figo hujiziba,kwa mujibu watafiti iyo kama mtu hato pata muda wa kupumzika ndivyo figo take itakavyo dhidi kupata athari.

Kwaiyo ili kuepuka athari iyo tunashauriwa pale ambapo tunakuwa hatupo bize kupumzika vya kutosha.

Share:

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Recent Posts