Home »
» Zijue dalili za ujauzito
Zijue dalili za ujauzito
DALILI ZA UJAUZITO.
Kukosa hedhi ni moja ya dalili au kiashiria cha uwepo wa mimba, kiashiria hiki hujitokeza takribani kwa wanawake wengi,dalili za ujauzito huweza tofautiana kati ya mwanamke na mwanamke mfano mwingine anaweza akatapika au kuhisi kichefuchefu sana lakini mwingine asipate kichefuchefu.
Kwaiyo kukosekana kwa hedhi pekee siyo uthibitisho wa uwepo wa mimba, hivyo basi ni lazima mwanamke afanyiwe vipimo ndivo vitathibitisha uwepo au kutokuwepo kwa mimba hii husaidia kutofautisha ujauzito na matatizo ambayo dalili zake hufanana na za dalili za ujauzito.
Dalili za ujauzito kwa ujumla wake ni kama ifuatavyo hapo chini.
.Mama kuhisi kichefuchefu na kutapika.
.Kujisikia kizunguzungu mara kwa mara.
.Kupata maumivu ya kichwa.
.Kukojoa mara kwa mara kuanzia wiki ya 6 hadi ya 14.
.Rangi ya ngozi kuzunguka chuchu huwa nyeusi zaidi kuliko ilivokuwa awali.
.Tumbo huongezeka ukubwa.
.Kupata choo kigumu.
.Kuongezeka uzito.
.Kuvichukia baadhi ya vyakula na kutamani aina fulan ya vyakula.
.Uchovu.
.Maumivu ya matiti.
.Mstari mweusi huone kana tumboni chini ya kitovu
.Kucheza kwa mtoto tumboni.
.Kusikia mapigo ya moyo ya mtoto.
.Kuonekana kwa mtoto kwenye kipimo cua utrasound.
.Kipimo cha mimba kuwa chanya.
Dalili tajwa hapo juu zimegawanyika katika makundi matatu nazo ni.
.Dalili ambazo huzihisi mama pekee.
.Dalili ambazo huonekana na watu wengine(mtu anaye mchunguza).
.Dalili ambazo huthibitishwa na uwepo wa vipimo.
Soma,kwanini-uendelee-kuteseka-na-ugonjwa.html
DALILI AMBAZO HUZIONA MAMA.
Haya ni mabadiliko au ishara ambazo mama mwenyewe pekee huziona au kuhisi, dalili hizi zaweza jitokeza nje na ndani ya mwili wa mama, dalili hizo ni kama.
.Mabadiliko katika maziwa kuanzia wiki ya 3,4 na kuendelea.
Katika kipindi hiki ngozi ya mama ambayo inazunguka chuchu zake huanza kua nyeusi zaidi ukilinganisha na vile ambavyo ili kuwepo kabla, licha ya kubadilika rangi maziwa ya mama pia huongezeka ukubwa au huanza kujaa. Weusi katika maziwa ya mana hudumu hadi muda wa kujifungua kisha hupotea taratibu.
.Kukosekana kwa hedhi kuanzia wiki ya nne na kuendelea.
Kukosekana kwa hedhi ni moja wapo ya dalili au kiashiria cha kwanza cha ujauzito,wanawake wengi pia huangalia hedhi kama ishara ya kushika mimba, kukosekana kwa hedhi siyo kwamba huashiria uwepo wa mimba hapana, kukosa hedhi pia kunaweza ashiria uwepo wa matatizo mengine e ambayo ni pamoja na kutokuwa na uwiano saw wa vichocheo mwilini,kuwepo kwa mimba ya uwongo, Msongo wa mawazo pia waweza sababisha kukosekana kwa hedhi na matatizo mengine mengi,kwaiyo wanawake wanashauriwa kuthibitisha kwa vipimo uwepo wa mimba licha ya kukosekana kwa hedhi.
.Homa wakati wa asubuhi kuanzia wiki ya 4 hadi14.
Kwa asilimia kubwa wanawake wengi hukutana na hali hii wawapo wajawazito, mjamzito huhisi kuchokachoka wakati wa asubuhi jambo ambalo husababisha kutokutamani kujishughulisha na shughuli yoyote na pengine kujikuta amelala siku nzima.,pia katika kipindi hiki wanawake wengi huwa hawapendi usumbufu, kwaiyo kwa kutambua ilo mwanaume inabidi kumchukulia mwenzio hivyo alivo, usiwe mwepesi kukasirika kwasababu siyo yeye ndo amependa hali hiyo itokee.
.Kukojoa kojoa mara kwa mara kuanzia wiki ya 6 hadi 12
Katika kipindi hiki mama hujihisi kukojoa kojoa mara kwa mara na pengine anaweza akapata au asipate mkojo, hali hii kitaalamu hutokana na kuongezeka kwa ukubwa wa mtoto tumboni, kadiri mtoto anavyokua tumboni husababisha mkandamizo kwenye kibofu cha mkojo jambo ambalo husababisha mama kuhidi mkojo umejaa kwenye kibofu na ivo kwenda kukojoa,licha ya kuongezeka kwa ukubwa wa mtoto hali hii pia inaweza ikasababishwa na mahonjwa mengine magonjwa ayo ni pamoja na UTI, kwaiyo ni vema kufanya vipimo ili kujiridhisha ni mjamzito au magonjw mengine ndo yamesababisha iyo hali.
.Kucheza kwa mtoto kuanzia wiki ya 16 hadi 20 nakuendelea.
Kucheza kwa mtoto ni moja ya ishara ambazo huashiria uhai wa mtoto, kwa kawaida mtoto hana idadi kamili ya kucheza tumboni mwa mama akd, lakini inashauriwa mtoto acheze japo mara kumi kwa siku,lakini kumbuka pindi utakavyo ona mtoto amepunguza kucheza au hachezi kabisa ni vema kwenda hospitali ukafanyiwe vipimo..
DALILI AZIONAZO MCHUNGUZI.
Hivi ni viashiria ambavyo mchuchuzi huviona aukuvigundua kutoka kwa mama baada ya kumfanyia uchunguzi, uwepo wa dalili tajwa hapo chini huashiria uwepo wa mimba.
.Uwepo wa kichocheo (hcg) chenye kuthibitisha uwepo wa mimba.
Kichocheo cha human chorionic gonadotrophin huanza kuonekana kwenye mkojo kuanzia siku ya 14 tangia mimba itungwe, pia kwenye damu huonekana kuanzia siku ya 9 hadi 10 tangia kutungwa kwa mimba kwaiyo mchunguzi baada ya kufanya kipimo kama kichocheo hiki kitaonekana basi nidhahiri mimba itakuwa imetungwa.
DALILI ZISIBITISHWAZO NA KIPIMO.
Uchunguzi kwa vipimo ndio pekee huthibitisha uwepo wa ujauzito, vipimo huthibitisha.
.Kusikia mapigo ya moyo ya mtoto.
.Mtoto kuonekana kwenye kipimo cha utrasound kuanzia wiki ya sita.
.Kuhisi kugusa viungo vya mtoto pindi uchunguzi wa tumbo unapofanyika.
.Kuongezeka kwa ukubwa wa mimba siku hadi siku.
No comments:
Post a Comment